Breaking News

SHEIKH JALALA ASHIRIKI HAFLA YA BARAZA LA EID El FITR JIJINI DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbambali wa dini na kiserikali mara baada ya kuwasili katika Baraza la Eid Al-Fitr katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika Baraza la Eid Al-Fitr lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) leo hii, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Mufti wa Tanzania Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir  Akizungumza katika Baraza la Eid Al-Fitr katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulama Sheikh Hemed Jalala, akisalimiana na Viongozi mbalimbali katika Baraza la Eid Al-Fitr lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) leo hii, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere



Dar es Salaam – Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulama Sheikh Hemed Jalala, ameshiriki katika Baraza la Eid Al-Fitr lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) leo hii, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.

Baraza hilo ambalo Mgeni alikuwa Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, sambamba na viongozi mbalimbali wa kidini na wa Serikali. Miongoni mwa malengo ya baraza hili ni kuimarisha mshikamano wa kidini na kuenzi maadili ya amani na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Aidha, Sheikh Jalala amepata fursa ya kuzungumza na viongozi mbali mbali, ikiwa ni pamoja na Balozi wa Saudi Arabia nchini, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Baraza la Eid. Ushiriki wake umeonyesha mshikamano na ushirikiano wa kidini nchini na kuthibitisha nafasi ya Jumuiya ya Shia katika shughuli za kidini za taifa.

Shughuli za Eid Al-Fitr zinaendelea kushikilia umuhimu mkubwa nchini, zikilenga kukuza mshikamano, amani, na maadili ya kiimani miongoni mwa wananchi wa Tanzania.