Breaking News

SHEIKH JALALA: QUDS NI MSINGI WA WATU HURU

Kiongozi mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Quds Duniani ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani katika Masjid Ghadiir Kigogo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Cha Jamia Al Mustafa International Sayyid Arif Naqvi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Quds Duniani ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani katika Masjid Ghadiir Kigogo jijini Dar es salaam.


Dar es salaam - Kiongozi mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala ametoa wito kwa Waislamu na watu wote wapenda haki juu ya wajibu wa kusimama na kuutetea msikiti mtukufu wa Quds na haki za watu waliodhulumiwa

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Quds Duniani yaliyofanyika Masjid Ghadiir Kigogo Post sheikh Jalala amesema lengo la maadhimisho ya Siku hii adhimu lengo lake ni kutangaza amani, umoja na mshikamano duniani 
"Majlisi hii inalenga kuwakumbusha Waislamu na watu wote wapenda haki juu ya wajibu wa kusimama na kuutetea msikiti mtukufu wa Quds na haki za watu waliodhulumiwa". Alisema Sheikh Jalala.

Alisema Kuadhimishwa kwa Siku hii kubwa na Adhwim ni kutangaza Utu na Ubinadamu na kuenzi Umoja wa Waislamu na kuitangazia Dunia Amani na Utulivu.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa kidini na kaulimbiu ya siku ya Quds mwaka huu 2026 yamebeba ujumbe wa "QUDS NI MSINGI WA WATU HURU"