Breaking News

DC MPOGOLO AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KWA KUDUMISHA AMANI

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto), akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Word of Reconciliation Church (WRC), Nabii Nicolous Suguye, wakati wa maadhimisho ya miaka 19 ya kanisa hilo. Katikati ni Askofu wa Kanisa la Arise Shine Ministry, Boniface Mwamposa.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewapongeza viongozi wa dini, katika mkoa Dar es Salaam kwa kudumisha amani katika nchi na kuleta maendeleo. 

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo,alisema hayo Dar es Salaam katika madhimisho ya kumbukumbu ya miaka 19 ya Kanisa WRC Kivule Wilayani Ilala ambapo ,alimwakilisha Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila .

"Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa dini kwa mchango wenu mkubwa wa kudumisha amani pamoja na kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu. Alisema DC Mpogolo 
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, alisema licha ya changamoto mbalimbali viongozi wa dini wanaendelea kujitoa kwa kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali kwa ajili ya mchango wao.

Mpogolo alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuleta maendeleo katika nchi na fursa mbalimbali za kiuchumi na utoaji fedha nyingi katika mkoa huo ambapo mafanikio hayo yote yamepatikana kwa ya viongozi wa dini kudumisha amani 
Alisema viongozi wa dini wamekuwa nguzo muhimu katika kuleta amani,utulivu,upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi na kujenga jamii kupitia hofu ya Mungu hali inayochangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa malengo ya Serikali .

Wakati huo huo kwa upande Mwingine Mpogolo aliwataka waumini na Wananchi kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu pamoja na kudumisha amani nchi yetu ya Tanzania.