MAKONDA : UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO "BOX" WALA "SUFURIA"
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema uwanja wa michezo unaojengwa Arusha ni miongoni mwa viwanja bora barani Afrika, ukiwa na muundo wa kipekee unaoakisi uhalisia wa maisha na jiografia ya Tanzania.
Makonda ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, iliyofanyika leo Aprili 17, 2026, kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya michezo kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
Ameeleza kuwa tofauti na viwanja vingine vinavyojengwa kwa miundo ya kawaida, uwanja huo umebuniwa kwa ubunifu unaoendana na mazingira ya Tanzania.
Amefafanua kuwa msukumo wa ubunifu huo umetokana na Mlima Kilimanjaro, utamaduni wa Wamaasai, madini ya Tanzanite pamoja na rangi za bendera ya Taifa.
Tbc Online




