Breaking News

VIJANA WAPATA FURSA KUBWA KUPITIA JUHUDI ZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema kuwa Vijana nchini wamepata baraka na bahati kubwa kupitia juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hasa kwa kutambua umuhimu wao na kuanzisha Wizara maalum inayoshughulikia masuala ya vijana.

Akizungumza katika kongamano la vijana lililofanyika jijini dar es salaam DC Mpogolo amewahimiza Vijana kuchangamkia vyema fursa zilizopo kwa kufanyia kazi ujuzi na vipaji walivyonavyo kama chachu ya kufikia malengo yao.
Awali akimkalibisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya alisema "Halmashauri yetu inaendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato huku ikiimarisha uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wananchi na hasa kundi maalumu la Vijana".

Aidha bw. Mabelya aliongeza kuwa vijana wanapaswa kutumia mikopo na mitaji wanayopewa kama nyenzo ya kuongeza ubunifu na mafanikio, huku akisisitiza kuwa changamoto zisichukuliwe kama kikwazo bali sehemu ya kujifunza na kufikia mafanikio.

Kongamano hili limekua na muitikio likiwakutanisha Vijana wengi kutoka kata 36 za Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam likiwa na kaulimbiu inayosema "Vijana Tuyajenge Tanzania ni Yetu".