Breaking News

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA EID EL-ADH'HAA MEI 27

Na Heri Shaban – Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) imetangaza kuwa Sikukuu ya Idd el-Adh’ha mwaka huu, kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu, itaadhimishwa Mei 27, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Alhaj Nuhu Jabiri Mruma, amesema swala ya Idd mwaka huu itafanyika kitaifa mkoani Dar es Salaam Mei 27, siku ya Jumatano, katika Msikiti wa Mfalme Mohamed IV uliopo Makao Makuu ya BAKWATA, wilayani Kinondoni.

Alhaj Mruma amesema swala ya Idd itaanza saa 1:30 asubuhi na baadaye kufuatiwa na Baraza la Idd mara baada ya kumalizika kwa swala hiyo.

Aidha, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar bin Zuberi bin Ally Mbwana, amewatakia Waislamu wote nchini maandalizi mema ya Sikukuu ya Idd el-Adh’ha.