WATUMISHI HALMASHAURI YA KISARAWE NA JWTZ WATOA MISAADA SHULE YA MSINGI KIKWETE NA KIBUTA SEKONDARI
Kisarawe - Watumishi halmashauri ya wilaya Kisarawe leo 22/05/2026 wametoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibuta na shule ya msingi kikwete,
Akizungumza kwa Niaba ya Watumishi halmashauri ya wilaya Kisarawe Waliofika kutoa msaada huo Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya Kongamano la wanawake Watumishi Kisarawe Bi Anita Rezaurwa alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na uhujitaji wa vifaa hivyo kwa wanafunzi hao walio katika mazingira Magumu kikwete na Kibuta,
Sisi kwa umoja wetu Watumishi tuliamua kwa kuchangangishana kidogo kidogo ili kuwapatia wanafunzi Hawa mahitaji haya licha ya kuwa kidogo lakini Imani yetu itafaa kwao” alisisitiza Bi Anita
Aidha alifafanua kuwa walishikiana na maafisa mbalimbali kutoka jeshi la wananchi JWT kambi ya Kisarawe kuweza kupata misada hiyo ya Leo,
”Hii misaada sio peke yetu Watumishi Kisarawe pia tulishiriana na wenzetu mbalimbali katika utumishi wa umma kupata zawadi hizi kwa wanafunzi wetu hawa natoa Wito jamii iungane katika kuwapatia wanafunzi wetu misaada mbalimbali Kama madaftari, taulo ili wafanye vizuri Shuleni” alitoa Bi Anita
Vifaa mbalimbali vilitolewa Kama madaftari, Uniform shati na Sketi na Kaptula na viatu,taulo za kike na sabuni kwa wanafunzi hao Kibuta na kikwete.
Akitoa neno la shukran kwa Watumishi wa halmashauri ya wilaya Kisarawe na JWTZ Kisarawe Mwalimu wa shule ya Msingi Kikwete Mwalimu Justine Mrutu,
”Nawashukuru Sana waliotoa na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu kuwabariki Sana kwa kutoa msaada huuu ambao unaenda kuwasiriti na kuwasaidia wanafunzi wetu Kisarawe lakini nawaomba mrudi Tena kuja kuwasaidia wanafunzi wetu maana wanahitaji msaada wenu”alisema Mwalimu Justine Mrutu.







