KATAMBI AWAHAKIKISHIA WATANZANIA KUENDELEA KUFURAHIA AMANI NA UTULIVU NCHINI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewahakikishia Watanzania kuendelea kufurahia amani na utulivu nchini, huku akiwataka kuendelea kushiriki shughuli za kiuchumi na maendeleo bila hofu.
Katambi ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Kozi Na. 6/2026 katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chogo, wilayani Handeni, mkoani Tanga, ambapo jumla ya askari 1,000 wamehitimu mafunzo hayo.
Amesema vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kuhakikisha amani na usalama wa nchi vinaendelea kuimarika, ikiwemo kukabiliana na taarifa mbalimbali zinazochochea uvunjifu wa amani kupitia mitandao ya kijamii, zikiwemo zinazohusu maandamano yanayodaiwa kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri askari hao 1,000, huku akibainisha kuwa taratibu zote za ajira kwa wahitimu hao zimekamilika.




