RAIS WA NAMIBIA AKITEMBELEA MAJIRANI ZAKE WA MAGOMENI - DSM
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, ametemebelea eneo la magomeni katika nyumba aliyowahi kuishi wakati wa harakati za ukombozi wa Namibia kupitia chama cha SWAPO.
Katika ziara hiyo ya kipekee iliyochanganya hisia za kumbukumbu na mshikamano wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, Rais Nandi-Ndaitwah amepokelewa kwa furaha na majirani zake hao wa Magomeni, akiwemo mama Salehe na mtoto wa mama Salama ambao walimfahamu tangu alipokuwa akiishi eneo hilo akiwa mwakilishi wa harakati za ukombozi.
“Magomeni ni sehemu ya maisha yangu na historia ya taifa langu. Tanzania ilitupa hifadhi, upendo na nafasi ya kupigania uhuru wetu. Huu ni ushahidi wa urafiki wa kweli na mshikamano wa Afrika,” amesema.








