TANESCO YAELEZA SABABU YA KUKATIKA KWA UMEME, UREJESHAJI WAANZA KWA AWAMU
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautaarifu umma kuwa leo Juni 27, 2026, majira ya saa 1:00 usiku, kumetokea hitilafu ya kiufundi katika Mfumo wa Gridi ya Taifa ya umeme, hali iliyosababisha mikoa yote inayopata huduma kupitia gridi hiyo kukosa umeme.
Shirika hilo linaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme kwa awamu katika maeneo yaliyoathirika ili kuhakikisha huduma inarejea katika hali ya kawaida.
Aidha, TANESCO imewaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwashukuru kwa uvumilivu wao wakati kazi za kurejesha huduma zikiendelea.




