Breaking News

ADO SHAIBU AANZA ZIARA YA SIKU MOJA PEMBA

PEMBA, Agosti 29, 2026 — Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amewasili kisiwani Pemba kwa ziara ya siku moja, ambapo amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kojani, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuimarisha uhai wa Chama.

Katika ziara hiyo, Ado Shaibu anatarajiwa pia kufungua matawi mapya ya ACT Wazalendo katika Jimbo la Pandani, Wilaya ya Wete, pamoja na Jimbo la Mtambwe.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha shughuli za Chama, kuongeza ushiriki wa wanachama katika shughuli za kisiasa na kujenga msingi imara wa ACT Wazalendo katika maeneo mbalimbali ya Pemba.

Ado Shaibu ameanza ziara hiyo leo, Agosti 29, 2026, kwa kushiriki shughuli za Chama katika Jimbo la Kojani kabla ya kuendelea na ratiba nyingine katika maeneo yaliyopangwa.