𝗪𝗜𝗭𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗬𝗔𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜 𝗠𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗢 𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗠𝗔𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔 𝗪𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗝𝗔𝗡𝗝𝗔 𝟮𝟬𝟮𝟲 𝗕𝗘𝗜𝗝𝗜𝗡𝗚
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir ameongoza timu ya wataalamu kutoka Wizara hiyo katika Mkutano wa Kimataifa Beijing, China (Global Smart Education Conference 2026 – GSE2026)
Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali kuhusu matumizi sahihi ya Akili Unde na STEM katika Elimu (AI and STEM Education).
Eneo kubwa majadilino likiwa kuzipa uwezo shule kuanzia shule za awali kuwa wabunifu kupitia matumizi sahihi ya AI katika mnyororo mzima wa thamani katika kutoa huduma ya elimu.
Mkutano huo umeanza tarehe 18 Agosti 2026, ukiwa na kaulimbiu “Akili Unde (AI) na Maendeleo Endelevu katika Elimu”.
Wakati Akili Unde (AI) inaendelea kutumika katika maendeleo Tanzania haitabaki nyuma katika mabadiliko hayo ambao tayari imeshaweka uelekeo kupitia Mkakati wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika elimu msingi 2024/25 - 2029/30 na Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Akili Unde kwenye Elimu (National AI Guidelines in Education).
Mikakati hiyo inainisha mbinu za kufundishia na kujifunzia darasani, matumizi ya maudhui yanayotumia AI, kuwajengea uwezo walimu katika matumizi ya Akili Unde, matumizi ya Akili Unde katika utafiti na maendeleo.








