WAZIRI MAVUNDE AITAKA GST KUTOKA OFISINI NA KUWAFUATA WACHIMBAJI MIGODINI
# Ampongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuiwezesha Sekta ya Madini katika Utafiti.
# Aitaka Bodi ya GST kuja na mawazo mapya yatakayosaidia utendaji kazi wa Taasisi.
# Aitaka Bodi kuifanya GST kuwa kinara wa utafiti wa madini na utoaji wa taarifa za jiosayansi Kusini mwa Jangwa la Sahara.
DODOMA - Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameiwataka Watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kutoka Ofisini na kuwafuata wachimbaji wadogo wa Madini ili kuwasaidia katika shughuli zao za uchimbaji na upatikanaji wa taarifa sahihi za kijiolojia.
Hatua hiyo inaenda sambamba na mkakati wa Serikali wa kuongeza kiwango cha tafiti za kina za madini nchini ili kubaini maeneo mapya yenye rasilimali za madini, kuongeza uwekezaji na kupunguza utegemezi wa uchimbaji wa kubahatisha.
Rai hiyo imetolewa leo Agosti 27, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Madini *Mhe. Anthony Mavunde* wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya GST, ambapo amesema kuwa katika kulipeleka taifa katika uchumi wa dola trilioni moja, GST inatakiwa ifanye utafiti wa jiolojia katika kilomita za mraba 50,000 ndani ya Quarter Degree Sheet (QDS) 20 ambazo sawa na asilimia 5 ya nchi nzima.
Aidha, Waziri Mavunde ameitaka Bodi ya GST kusimamia na kushauri katika utafiti wa QDS 23 kwa lengo la kuongeza taarifa mpya za rasilimali madini nchini kutoka asilimia 16 zilizopo sasa hadi 21 ifikapo mwaka 2030.
Pia, Waziri Mavunde ameielekeza Bodi ya GST kuhakikisha kuwa, wataalam wa GST wanatumia mifumo ya teknolojia ya kisasa katika utunzaji wa taarifa za jiosayansi ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani yanayowezesha upatikanaji wa taarifa kwa wakati na usahihi.
Kwa upande wake, Naibu waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa ameitaka GST kufanya shughuli zake za utafiti kwa kushirikiana kwa ukaribu na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili kuendelea kubaini maeneo mapya yenye madini katika nchi na kuendeleza maeneo ambayo tayari yana taarifa za upatikanaji wa madini.
Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Bw. Msafiri Mbibo amesema katika kipindi cha miaka 100 GST imefanikiwa kufanya mambo makubwa










