𝗪𝗔𝗖𝗛𝗜𝗠𝗕𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔𝗗𝗢𝗚𝗢 𝗪𝗔𝗞𝗔𝗕𝗜𝗗𝗛𝗜 𝗛𝗔𝗧𝗜 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗨𝗞𝗥𝗔𝗡𝗜 𝗞𝗨𝗜𝗦𝗛𝗨𝗞𝗨𝗥𝗨 𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗣𝗔𝗧𝗜𝗔 𝗟𝗘𝗦𝗘𝗡𝗜
Viongozi wa Kikundi cha Jeraphi Miners cha Nyangh'wale mkoani Geita wamemshukuru Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuwapatia Leseni ya Uchimbaji Madini kupitia Wizara ya Madini.
Akiwasilisha hati hiyo mbele ya Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde Mwenyekiti wa Kikundi hicho Ndg. Elias Ndani ameishukuru serikali kwa utatuzi wa mgogoro wa eneo la Ifugandi na kwa kuwapatia Leseni ya uchimbaji eneo la Kwimba,Mkoani Mwanza.
Akipokea hati hiyo,Waziri Mavunde amewapongeza wachimbaji hao wadogo kwa moyo wa shukrani na kuwataka kuzalisha kwa tija ili kuchochea uchumi kupitia sekta ya madini.






