DCEA YAKAMATA PAKITI 299 ZA HEROIN, METHAMPHETAMINE MWENGE
Dar es salaam - Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watu wanne na paketi 299 za dawa za kulevya, zikiwemo heroin 24 na methamphetamine 275, katika operesheni iliyofanyika Novemba 6, 2026, eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Dawa hizo zilikamatwa zikiwa zimefichwa ndani ya magari mawili aina ya Ford Ranger yenye namba za usajili T.950 ERA na T.417 EJZ, ambayo pia yanashikiliwa na mamlaka kutokana na kuhusishwa na tukio hilo.
Watuhumiwa waliokamatwa ni Juma Slaati Kisomeko (36), raia wa Uganda, dereva na mkazi wa Piji nchini humo; Issa Said Nassoro (34), mfanyabiashara; Ibrahim Said Chembela (30), dereva; na Mohamed Ally Shemtuu (45), dereva.
Watuhumiwa watatu ambao ni Nassoro, Chembela na Shemtuu ni wakazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam.
Operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi za DCEA katika kudhibiti na kupambana na biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya nchini.









