Breaking News

WAZIRI MKUU APONGEZA HATUA ZILIZOFIKIWA KWENYE UTAFITI, AELEKEZA KUFIKIA MAENEO MENGINE ZAIDI

Dar es salaam - Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwingulu Nchemba, ameipongeza Wizara ya Madini kwa jitihada za kufanya tafiti zinazolenga kuongeza uelewa wa rasilimali za madini nchini na kuimarisha tija katika Sekta ya Madini.

Akizungumza katika hafla ya Usiku wa Madini iliyofanyika jijini Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mlimani City, Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kuendeleza tafiti hizo katika maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa, ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa taarifa za jiolojia na fursa za uwekezaji katika sekta hiyo.

Alisema ni muhimu nguvu kazi na utaalamu wa wataalamu waliopo nchini kutumika ipasavyo katika kuendeleza shughuli za utafiti, kubaini maeneo yenye uwezekano wa kuwa na rasilimali za madini na kutoa taarifa sahihi zitakazowawezesha wadau kufanya maamuzi yenye tija.
Aidha, alisisitiza kuwa kuendeleza tafiti za madini katika maeneo mbalimbali nchini kutasaidia kuongeza thamani ya rasilimali zilizopo, kuchochea uwekezaji, kukuza shughuli za uchimbaji na kuimarisha mchango wa Sekta ya Madini katika uchumi wa taifa.

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu alifafanua kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa maendeleo ya Sekta ya Madini kupitia maboresho ya sera, sheria, kanuni na miongozo inayolenga kuimarisha shughuli za utafiti, uchimbaji na uchenjuaji wa madini nchini. Amesisitiza kuwa mkazo unawekwa katika kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi ili rasilimali hizo ziwe na mchango mkubwa zaidi katika kukuza uchumi na kuongeza manufaa kwa Watanzania.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha tafiti za kina za madini kwa kutumia utaalamu na teknolojia za kisasa, hatua itakayosaidia kubaini maeneo mapya yenye uwezekano wa kuwa na madini, kupanua wigo wa shughuli za uchimbaji na kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo. Amesema kuendeleza tafiti hizo ni msingi muhimu wa kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa ufanisi na kuleta tija kwa taifa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kushirikiana na Tanzania katika shughuli za utafiti, uchimbaji na uongezaji