SALMA JABU (NISHA), KULA FUTARI NA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI DAR
Mwigizaji wa filamu za kitanzania
Bi, SALMA JABU maarufu kama (Nisha) ameandaa futari kwa watoto waishio
katika mazingia hatarishi waishio jijini dar es salaam siku ya tarehe 26 mwezi
huu.
Akizungumza
na wandishi wa habari leo juu maandalizi amesema futari imewalenga zaidi watoto
wanaoishi katika vituo vya kulelea yatima pamoja na wale ambao wapo mitaani
hawana sehem maalum ya kuishi inataji kufanyia katika viwanja vya shule ya
sekondari ya Azania jiji da es salaam.
“Katika kuhakikisha watoto wanaishi katika mazingira magumu nao wanashiriki
kikamilifu katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan ameona ni vema
kuwaandalia futari hili nao wanashiriki vyema katika kipindi chote cha mfungo
kama watoto wengine”
Amesema
kufata nguzo za dini ya kiislam, kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, waislam wanapswa kutoa Dhaka pamoja na kuonyesha upendo kwa wengine hususani
walio katika mazingira magumu hasa watoto yatima, watoto wenye ulemavu wa
ngozi,walemavu pamoja na watu wenye mahitaji maalum hili kuweza kuwafanya
wapate faraja kubwa nao.
Aidha
msanii huyo bi, SALMA JABU (Nisha) ameongeza kuwa hafla hiyo ya futari
inatarajiwa kuzuliwa na makamu wa rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania
mhe SAMIA SULUHU HASANI, Mbunge wa jimbo la Ilala MUSSA ZUNGU, Mkuu wa
mkoa wa dare s salaam PAUL MAKONDA, viongozi wa dini pamoja na wasanii
mashuhuri.



