WATANZANIA WAPATA FURSA YA KUSHIRIKI MAFUNZO KUHUSU TSUNAMI
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito
Kodijat akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo
ambayo watapatiwa
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akitoa neno
la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na kueleza sababu ya kufanyika
mafunzo hayo.
Mkuu
wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa nchini
(TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga kuendeleza
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka Watanzania kuwa na
utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa katika kipindi hiki
ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard
Chamuriho akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yanayohusu kuwapa elimu
washiriki ya kuhusu Tsunami.
Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
……………………………………………………………………………………………………………
Kutokana na kuwa na athari
kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa, Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali
nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.
Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema
kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na
Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni
matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa
Watanzania wengine.
“Watu wengi wamepoteza maisha
tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha
kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani
Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa,” alisema
Bi. Rodrigues.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema
kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa
yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo
lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na
kusababisha vifo vya waogeleaji watano.
“Mafunzo haya yanatakiwa
kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na
yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku
athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua
athari za Tsunami hata likitokea mbali,” alisema Dk. Chamuriho.



