WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI 2016 KWA KUSIKILIZA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Dkt. Yamungu Kayandabila akisisitiza jambo kwa
watumishi wa wizara hiyo, alipokutana nao katika Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2016. Dkt Yamungu alipokea kero mbalimbali kutoka kwa
watumishi hao pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza ufanisi katika
utoaji wa huduma kwa wananchi.
Baadhi
ya watumishi na watendaji wa Wizara ya Ardhi, wakimsikiliza Katibu Mkuu
Dtk. Yamungu akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwake na
watumishi hao kama sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
2016.
Mtumishi
Beatus Kashangaki akitoa kero zake kwa Katibu Mkuu Dkt. Yamungu
Kayandabila wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.



