RAIS MSTAAFU WA KENYA, MWAI KIBAKI ATEMBELEA DARAJA LA MWALIMU NYERERE.
Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Maji Afrika (Sylivester Matemu) wakati
wa maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini
Dar es salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki akisalimia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo leo jiji Da es salaam.
Katibu wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi
akifafanua jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu
Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na
eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.
Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi walioandamana kutembelea daraja la Mwalimu Nyerere
linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la
katikati ya jiji la Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………………….
Mwakilishi Maalumu wa masuala ya
maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki
ametembelea mabanda ya maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika
yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Katika tukio hilo Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo
amimweleza Mwakilishi huyo kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa
hadi ifikapo 2020 iweze kufikisha maji kwa wananchi wote kwa maendeleo
yao na taifa kwa ujumla.
Mhandisi Kalobelo aliongeza kuwa
hatua hiyo itaifanya Tanzania kufikisha maji kwa wakazi wa mijini kwa
asilimia 95 na kwa wakazi wa vijijini kw asilimia 85.
Aidha, katika hatua nyingine,
Mwakilishi huyo alitembelea barabara iliyopewa jina la Mwai Kibaki
inayoanzia eneo la Morocco hadi njia panda ya Kawe jijini Dar es salaam
pia alitembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la
Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es
salaam.
Maonesho ya sita katika ya wiki ya
maji Afrika mwaka huu yanayoendelea jijini Dar es salaam yanaongozwa na
kaulimbiu inayosema “Kufikia lengo la Mendeleo Endelevu (SDGs) juu ya
Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira”.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)



