Breaking News

MZEE WA UPAKO: VINGOZI EPUKENI VIJEMBE KATIKA MIKUTANO,



Mchungaji wa kanisa la Maombezi (CRG), Antony Lusekelo (mzee wa upako)


Mchungaji kiongozi wa Kanisa La Maombezi (CRG), Antony Lusekelo (maarufu mzee wa upako) amewataka viongozi wa Kisiasa hapa nchini kuacha tabia ya kupigana vijembe katika mikutano yao ya chama badala yake wajikite katika kutibu majeraha ya uchaguzi wa mwaka jana kwa kuhubiri ushirikiano na umoja wa kujenga Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake jijini dar es salaam kwa lengo la kuzungumzia mwenendo wa hali ya Kisiasa hapa nchini mara baada ya kuisha kwa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini octoba mwaka jana.

Amesema si wakati wa kubeza baadhi ya watu waliohama chama kimoja kwenda kingine, kwani kufanya hivyo ni kuendelea kujenga chuki miongoni mwa jamii hali inayoweza kupelekea kupotea kwa amani ya nchi.

Tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu amekuwa akifuatilia mwenendo na matukio ya kisiasa hapa nchini na kuona kumeanza kujitokeza tabia ya kupigana vijembe miongoni mwa wanasiasa, kukejeli na kuwasema vibaya wenzao huo si utaratibu mzuri na si utamaduni wa Tanzania.

Amesema kwa sasa upinzani nchini umekuwa kwa kasi, na una wafuasi wengi hivyo vitendo vya kuendeleza vijembe vinaweza kupelekea kusababisha machafuko ambayo hayana ulazima wowote.

“Baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 nchi yetu bado haijatulia vyema, bado watu wanamajeraha makubwa ya uchaguzi mkuu, ni wakati wa kuponya majeraha hayo kwanza pamoja na kuendelea kuhubiri umoja”.

Aidha mchungaji lusekelo amezungumzia pia hatua ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni na kususia vikao vya bunge amesema kitendo kile kinalitia aibu taifa, hivyo kushauri busara itumike wazee wajitokeze na kukaa kuzungumza na pande zote mbili kwa lengo la kumaliza tofauti zao ili Taswira ya Taifa isiharibiwe.

“Amesema hakuna wa kulaumiwa kwa kilichotokea bungeni wote wanamakosa kuanzia wabunge wateule na hata Naibu Spika wa Bunge mhe Tulia Ackson, na kuongeza kuwa swala hilo limeshindwa kupatiwa suluhu kutokana na uchanga mhe naibu spika, kinachotakiwa wazee waingilie kati ili suluhisho lipatikane”.

Aidha mchungaji lusekelo ameongelea pia ujio wa kiongozi maarufu wa kiroho kutoka nchini Nigeria TB JOSHUA, kwa kutoa taadhari kwa serikali awamu ya tano kuacha kumpokea nchini mtumishi huyo wa kiroho kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha laana kubwa kwa Taifa la Tanzania ikiwemo kunyesha mvua sizizo fahamika.

Zipo taarifa kuwa kiongozi huyo wa kiroho TB Joshua anatarajiwa kuja tena nchini na kupokelewa na mhe Rais Magufuli, nataka nimwambie mhe Rais Magufuli kumpokea TB Joshua ni kuleta laana katika Taifa kwani mtumishi huyo cha ziada ambacho wachungaji wa ndani hawana.

Mchungaji Lusekelo ametoa taadhari kwa nchi kutompokea tena mhubiri kwani upo uwezekano wa kusababisha madhara makubwa sana nchi ikiwemo kutokea maafa makubwa kwa madai kuwa kiongozi huyo hana sifa ya kuwa mhuburi.