PAPA AMTIMUA KIONGOZI WA DINI KWA KUSAMBAZA KONDOMU

Kiongozi
wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta amejiuzulu kufuatia mgogoro na
Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya kondomu kulingana na kanisa hilo.
Mathew
Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka
kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi.
Hatua
hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa hilo huko Malta
lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la Myanmar.
Kanisa
katoliki linakataza utumizi wa mipira ya kondomu. Papa Francis alimtaka
ajiuzulu na alikubali. Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama ule wa taifa
zima. Hutoa pasipoti, stampu na leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia na
mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.



