RAIS TRUMP KUZUIA WAHAMIAJI KUTOKA NCHI ZA KIISLAMU AFRIKA NA MASHARIKI YA KATI,

Rais
wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini sheria kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia
nchini humo.
Taarifa
kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka
wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani
leo Jumatano.
Aidha,
anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa
kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu
wengi
Bw
Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama
wa taifa la Marekani.
Wakati
wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la
uhamiaji Marekani.
Aligusia
ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga
marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya
ugaidi.
Baadaye
alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni
kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.
Anatarajiwa
kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini
maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na
baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza
idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.
Na
hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba
ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya
waumini wa Kiislamu.
Ubaguzi
wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa
utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura
kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.
Awali,
Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu
cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.
Vyombo
vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na
wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.
Bw
Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la
mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.
Chanzo:
BBC



