UVCCM YATABIRI ANGUKO LA VYAMA VYA UPINZANI 2020
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kutokana na kushamili kwa
ubabe, udikteta na ung’ang’anizi wa
madaraka ipo siku viongozi wa upinzani wataondolewa kwa nguvu na aibu.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar es salaam
baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana kutathmini
ushindi wa uchaguzi.
Shaka
amesema kuwa watanzania wataendelea kuiamini CCM kwa mambo mengi, ikiwemo
kuleta uhuru na mapinduzi, sera, uongozi na utawala, kujali na kutazama maslahi
mapana kwa manufaa ya umma na pia tabia ya utii wa sheria na kuheshimu katiba
bila shuruti.
“Viongozi
ving’ang’anizi wa madaraka ya kisiasa ni hatari kukabidhiwa dhamana ya madaraka
na dola, ikitokea bahati mbaya siku moja wakapewa dhamana hiyo, hawatapisha
wengine na huo utakuwa ni mwanzo wa kutikisika misingi ya utaifa, mshikamano na
amani ya nchi,”amesema Shaka.
Aidha,
Shaka amesema kuwa inashangaza kuwaona viongozi wa kisiasa ,akiwemo Mwenyekiti
wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif wakijenga himaya
ndani ya vyama vyao huku wakidaiwa kufanya ubabe katika uongozi wao.
Hata
hivyo amesema kuwa ukandamizaji au kukosekana
kwa uhuru wa mawazo naDemokrasia ndani ya upinzani,ni kielelezo tosha
kuwa viongozi wake huimba kinadharia dhana ya demokrasia huku wakishindwa
kuonyesha kwa vitendo.




