Atimae Mugabe Ang'olewa Urais Zimbabwe

Emerson Mnangagwa
Mnangagwa alikuwa makamu wa rais
wa zamani wa nchi hiyo chini ya Rais Robert Mugabe.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama cha
ZANU-PF, inasemama Mnangagwa amefanywa kuwa rais wa mpito.
Hivi karibuni Mnangawa mwenye umri
wa miaka 75 alifutwa kama makamu wa rais kutokana na kile serikali ilisema kuwa
kutokuwa mtiifu.
Kufutwa kwake kulionekana kama nia
ya kumwezesha mke wa rais Mugabe, Grace kufuata nyayo za mumewe na kuwa
kiongozi wa Zimbabwe.
Awali alikuwa ametoa wito kwa
mumewe kumfuta makamu wa rais.
Mnangagwa ambaye ni mkuu wa zamani
wa ujasusi amekuwa mtu ambaye alitarajiwa kumrithi rais Mugabe 93.
Kufutwa kwake kulimaanisha kuwa
Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa kuwa makamu wa rais wakati wa mkutano maalum
wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi ujao.



