Wakili Manyama Aufagilia Utendaji Wa Rais Magufuli..Awasihi Wananchi Kumwunga Mkono.
Mkurugenzi wa Kampuni ya uwakili ya Smile Stars Attorneys, na wakaili wa kujitegemea Bw.Leonard Manyama amewaasa watanzania kupuuza kauli za wanasiasa ambazo wamekuwa wakizitoa katika majukwaa ya siasa kuponda utendaji wa serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli badala yake kuendelea kuunga mkono hatua ambazo amekuwa akizichukua kwa maslahi ya Taifa hasa wananchi wanyonge.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam juu
ya mafanikio na hatua zinazochukiliwa na serikali ya awamu ya tano kwa kipindi
cha miaka miwili chini ya rais Magufuli, wakili Manyama alisema kumekuwapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia
majukwaa ya siasa kubeza mafanikio na jitihada ambazo amekuwa akizichukua rais
hususani wizi wa asilimali za nchi.
“kumekuwepo na kikundi cha baadhi ya wanasiasa kutumia majukwaa na
mitandao ya kijamii kuponda hatua za dhati ambazo rais Magufuli amekuwa akizichukua
kuhakikisha analinda rasilimali za nchi, mapambano dhidi ya rushwa pamoja na
ufisadi ni wa kupuuzwa kwani awana nia njema na nchi yetu” Alisema Wakili
Manyama.
Wakili Manyama alisema ameitisha mkutano na waandishi wa habari kwa
lengo la kuchambua kisheria madai hayo potofu ya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa awana mapenzi mema na nchi
hivyo kuwataka wananchi kuwapuuza badala yake waendelee kumwunga mkono rais
Magufuli katika jitihada za dhati anazochukua kuwaletea maendeleo.
“Mafanikio ya rais Magufuli kwa kipindi cha miaka miwili tangu
kuchaguliwa kwake ni makubwa ikiwepo hatua madhubiti nazochukua Mapambano dhidi
ya rushwa na Ufisadi, kudhibiti ukwepaji kodi, Mapambano dhidi ya Ujangili,Usimamizi
dhabiti wa rasilimali za nchi sambamba na kuziba mianya ya ubadhilifu
Serikalini”. Alisema Wakili Manyama.
Aidha wakili Manyama ametolea ufafanuzi sababu za kupotea kwa pesa alisema kunatokana na hatua ambazo rais Magufuli amekuwa akizuchukua kupambana na
vitendo vya kiuharifu ambavyo ndiyo msingi wa utakatishaji wa fedha haramu ,
jambo ambalo limepelekea fedha ambazo zilikuwa zikipatikana ovyo kutondoka mtaani.
“Hatua ambazo mhe rais amekuwa akizichuka kupambana vitendo ambavyo
kimsingi wahusika walikuwa wanatumia mianya hiyo kujiufaisha na kujilimbikizia mali kisha fedha zinazokwa zikipatikna
kuziingiza katika mzunguko wa fedha jambo lilokuwa linapelekea kuwepo na fedha
nyingi haramu mitaani ivyo kufatia hatua za dhati za rais Magufuli kuziba mianya
hiyo ndio chanzo kilichopelekea fedha haramu kupotea” Alifafanua Wakili Manyama.



