Muhubiri Anayetumia Nyoka, Awalisha Mende Waumini Wake....Wenyewe Wachekelea

Muhubiri mashuhuri anayetumia nyoka
nchini Afrika Kusini Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili katika
mkusanyiko wa kanisa lake akidai kwamba wadudu hao walibadilika na kuwa jibini
kwa mmoja wao na kiungo kwa mwengine.
Kisa hicho kinajiri takriban miezi
mitano baada ya Mnguni katika ibada ilioandaliwa na Muhubiri wa Nigeria TB
Joshua, na kukiri kulingana na bwana Joshua kwamba kuwalisha watu haijaandikwa
katika biblia.
Kanisa la bwana Mnguni lilichapisha
katika mtandao wa facebook kuhusu kisa hicho cha kula mende mapema mwezi huu
akisema kuwa muhubiri huyo alimwita mende kuja katika kanisa hilo.
Baadaye aliwaita wafuasi wa kanisa
hilo kujitokeza mbele na kula....ndipo ndugu wawili walijitokeza na kula
pamoja...na walipokuwa wakila bwana Charles alihisi anakula jibini huku Bwana
Eric akihisi kula kiungo, chapisho hilo lilisema.
Huku akizungumza maneno haya ''uwezo
wa mungu uliwagusa wote wawili, kwa kuwa walipo'' , aliongezea.
Kanisa hilo pia liliripoti katika
chapisho jingine kwamba muhubiri huyo aliliombea uwa la sumu , na baadaye
mfuasi mmoja alilila ua hilo pekee na kulimaliza.
Nabii huyo aliyejitangaza alizua
utata nchini Afrika Kusini 2015 baada ya kushutumiwa kwa kuwalisha nyoka
wafuasi wake.
Mashtaka dhidi ya Mnguni
yaliowasilishwa na shirika la kuzuia ukatili dhidi ya wanyama ,yalitupiliwa
mbali mnamo mwezi Julai 2015 kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Chanzo-BBC



