Waziri Mkuu Aongoza Maombolezo Ya Kifo Cha Katibu Mkuu Wa CWT
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu
cha maombolezo alipo hudhuria msiba kwa aliyekua Katibu Mkuu wa Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa, leo Novemba 18, 2017
nyumbani kwa marehemu Toangoma, jijini Dar es salaam. Aliye simama kwa kwa
Waziri Mkuu ni Mke wake Mama Mary Majaliwa.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia,
Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha
aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu, Tuangoma
Jijini Dar es Salaam.
Bw. Msulwa
amefariki dunia juzi (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Hospitali ya Aga Khan
jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika maombolezo hayo
Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
Akizungumza kwa
niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa
sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni
zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Bi.
Sharifa Msulwa kufuatia kifo cha Mume wake aliye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) Marehemu Alhaji Yahya Msulwa . Waziri Mkuu alifika
nyumbani kwa Marehmu Toangoma jijini Dar es salam leo November 18, 2017.
Waziri Mkuu
amesema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi na mwenye ushirikiano mzuri na
wenzake, ambapo Novemba 12, 2017 alipokea barua kutoka CWT iliyosainiwa na
marehemu akimualika kushiriki kwenye shughuli za chama.
“Wote tumeguswa na
msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa Chama cha Walimu Tanzania
tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa kila mmoja. Alikuwa na tabia
njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema aliyotuachia”
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa,
akisaini kitabu cha maombolezo alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu
wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa. Aaliye simama
kushoto kwake ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa pamoja na Mke
wake leo Novemba 18, 2017 nyumbani kwa marehemu Toangoma, Jijini Dar es
salaam.
Waziri Mkuu
ameongeza kuwa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho
yake mahali pema. Nawaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto kuwa na moyo
wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.”
Marehemu
anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 18, 2017.






