KAULI YA POLEPOLE KUFATIA YA MBUNGE WA CUF KUJIUZULU NA KUTANGAZA KUHAMIA CCM

Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema Chama cha Mapinduzi (CCM)
hakitampokea yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata
utaratibu.
Kauli hiyo imekuja
baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF), Maulid Said Abdallah
Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia
kwenda CCM.
Polepole aliyasema
hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama.
“Ameamua kule aliko
haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba wawili huwezi kuwa
na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto watamsikiliza nani, basi
amehama,” alisema Polepole.
“Sasa mimi niko
hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais wetu ambaye ni
mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ikimpendeza
afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione vinaelea kwa mazuri yale
asione vimeshushwa vimeundwa na wanaounda mambo mazuri ya Magufuli ni Chama cha
Mapinduzi.”



