PICHA: BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA
Mbunge wa Segerea
Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo
lake katika bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali.
Bonanza hilo
lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabatalilikuwa ni
hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara
FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka
kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.
Mshindi wa fainali
alijishindia shilingi milioni moja
taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata shilingi laki tano na mshindi wa tatu
akiondoka na shilingi laki tatu.
Akizungumza baada
ya fainali Mheshimiwa Bonnah Kaluwa
amesema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila
mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi
wa mwaka huu atapata nafasi ya kwenda
Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea
Mh. Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla
ya mchezo wa fainali.
Mbunge wa Segerea
Mh. Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mheshimiwa Bonnah
Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani
wa Taifa Stars
Mshambuliaji wa
timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki
wakifuatilia mchezo
Wachezaji wa
Bodaboda Kimanga wakifurahia kombe lao
Mheshimiwa Bonnah
Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli











