KUTOKA SHINYANGA: ALIYETUMBULIWA KWA VYETI FEKI AJIUA

Mkazi wa Majengo wilayani Kahama mkoani
Shinyanga amejinyonga kwa kutumia kipande cha chandarua usiku wa kuamkia leo
akiwa kwenye chumba chake cha kupanga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugumu wa
maisha.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Said Ndago
amesema kuwa mdogo wake ambaye amejinyonga anaitwa Jumnne Said Ndago
ambaye alikuwa ameachishwa kazi ya Udreva katika halmashauri ya Msalala
kutokana na kutokuwa na vyeti.
Amesema kuwa kabla ya kujinyonga aliandika
Meseji kwa dada yake ambaye anafanya kazi Jijini Dar es salaam ambayo ilikuwa
inasema kuwa anamuomba amtunzie watoto wake kwani yeye hatakuwepo duniani .
Kwa upande wake jirani wa marehemu ambaye
walikuwa wanaishi nyumba moja Edward Nkondi amesema kuwa kijana huyo hakuwa
anashinda Nyumbani kutokana na kuwa mke wake wake alikuwa amekwenda kwao Tabora
hivyo alikuwa anaishi Peke yake hali ambayo ilikuwa ikichangia kutoshinda
Nyumbani.
Amesema kuwa alikuwa anafika kwake usiku ,
lakini pamoja na kufika kwake alikuwa haonyeshi dalili za kwamba angefanya
tukio kubwa kama hilo alilofanya la kujinyonga na kwamba alikuwa kijana mcheshi
na mchangamfu.
Naye mkuu wa kitenngo cha Upelelezi ndani ya
jeshi la Polisi mjini Kahama George Bagyemu kwa niaba ya Kamanda wa polisi
mkoani Shinyanga Simon Haule amekiri kupokea taarifa hiyo na kwamba tatizo la
kujinyonga ni ugumu wa maisha .



