MAHAFALI YA KWANZA YA MRADI WA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO KWA WATOTO YAFANA JIJINI DAR.
Mgeni Rasmi Afisa
Maendeleo ya Jamii Manspaa ya Temeke Bw, John Bwana Akizungumza Katika Mahafali
Ya Kwanza Ya Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) Mradi Ambao
Unaratibiwa Kupitia Shirika La Brac Tanzania 7 Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Mwakilishi Kutoka Shirika La Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Watoto UNCEF, Bi. Hafsa Khalifan Akiongea Katika Mahafali Ya Kwanza Ya
Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) Mradi Ambao Unaratibiwa Kupitia
Shirika La Brac Tanzania 7 Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Mtaalam Wa Maswala
Ya Watoto Na Makuzi Kutoka Shirika La Children In Crossfire Bi. Victoria
Lagygina Akizungumza Katika Mahafali Ya Kwanza Ya Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya
Mtoto (The Lego) Mradi Ambao Unaratibiwa Kupitia Shirika La Brac Tanzania 7
Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Meneja Wa Mradi Wa
Makuzi Na Malezi Kwa Watoto Kutoka Shirika La Brac Tanzania Bi. Janeth Malela
Akifafanua Jambo Katika Mahafali Ya Kwanza Ya Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya
Mtoto (The Lego) Mradi Ambao Unaratibiwa Kupitia Shirika La Brac Tanzania 7
Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Watoto Wakionyesha
Michezo Mbalimbali Kwa Mgeni Rasmi (Hayupo Pichan) Katika Mahafali Ya Kwanza Ya
Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) Mradi Ambao Unaratibiwa Kupitia
Shirika La Brac Tanzania 7 Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Watoto wakimsikiliza
mgeni rasmi Bw. John Bwana (hayupo pichani) wakati akiutubia katika Mahafali Ya
Kwanza Ya Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) Mradi Ambao
Unaratibiwa Kupitia Shirika La Brac Tanzania 7 Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Wazazi Na Walezi
Wakifatilia Hotuba Ya Mgeni Rasmi (Hayupo Pichani) Katika Mahafali Ya Kwanza Ya
Mradi, Makuzi Na Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) Mradi Ambao Unaratibiwa Kupitia
Shirika La Brac Tanzania 7 Decemba Jijini Dar Es Salaam.
Dar es salaam:
Serikali imesema
inatambua jitihada za mashirika na taasisi binafsi katika kusaidia na kuboresha
mazingira ya elimu nchini hususani kwa watoto ili kuwajenga kabla ya kuanza
elimu yao ya awali.
Akizungumza Katika Mhafali Ya Kwanza Ya Mradi, Makuzi Na
Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) Mradi Ambao Unaratibiwa Kupitia Shirika La Brac
Tanzania Afisa Maendeleo Ya Jamii Wa Manspaa Ya Temeke Bw. John Bwana kwa niaba
ya mkuu wa wilaya ya temeke alisema serikali inatambua na inaunga mkono
jitihada ambazo zimekuwa zikichukuliwa na wadau mbali mbali katika kuhakikisha
wanaboeresha mazingira elimu nchini hususani elimu ya awali kwa watoto.
“Elimu hii
waliopata watoto ni msingi mkubwa katika kuwaandaa na elimu ya awali ambayo
inawaimalisha watoto katika maendeleo ya kiakili, kimwili, kihisia na lugha”
alisema Bw. Bwana.
Bw Bwana Alisema kupitia
mradi huo wazazi wa watoto hao wamepatiwa mafunzo juu ya malezi bora kwa
watoto wao ambayo ni muhimu kwa makuzi ya watoto kwa sababu msingi wa ukuaji wa
mtoto huanzia kwa mzazi mwenyewe.
Alisema kupitia
mradi huo wa Makuzi Na Maendeleo Ya Mtoto (The Lego) wazazi na walezi wameshriki
kazi mbalimbali za mradi kama mikutano ya kuwajengea uwezo juu ya utengenezaji
wa vifaa vya asili kwa ajili ya watoto kutumia katika mafunzo yao.
Aidha Bw. Bwana
aliongeza kuwa kwa upande wa serikali mradi huu ni muhimu sana kutokana na
uwepo wa vituo ambavyo vinasaidia kuwapatia watoto fursa ya elimu ya makuzi na
malezi kama msingi katika awali.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Meneja wa mradi wa makuzi na malezi ya watoto kutoka
shirika la Brac Tanzania Bi. Janeth Malela alisema mradi huo ni shirikishi kutokana
na kushirikisha wazazi/walezi, viongozi wa serikali, wadau na wataalamu ambao
wamekuwa mchango katika utekelezaji wa mradi huu.
Alisema kutokana na
umuhimu na mafanikio ya mradi wa Play Lab, Brac kwa kushirikiana na serikali
wapo katika mchakato wa awali wa kupendekeza kuwepo na mtaala wa kufundishia
vituo hivi vya makuzi na malezi kwa watoto wadogo ambao itasisitiza pia ufundishaji
wa watoto kupitia michezo.
Jumla ya watoto
1200 (Mbeya 570 na Temeke 630) wamehitimu mafunzo ya miaka miwili ya makuzi na
malezi kupitia mwongozo wa mtaala wenye masomo ya Hesabu, Sayansi, Ubunifu, Kusoma
Na Kuandika Pamoja Na Lugha Ya Mawasiliano.














