Ridhwaa-Kinondoni Yaomba Wadau Kuchangia Ujenzi Wa Chuo
TAASISI ya Ridhwaa
ya Kinondoni ya Jijini Dar es Salaam Tanzania imewaomba wadau mbalimbali
waelimu na watanzania wenye uzalendo kujitokeza kuchangia mpango wa ujenga chuo Kikuu kitakacho
gharimu Shilingi bilion mbili za kitanzania
ikiwa ni moja ya mikakati yao kama taasisi katika kueneza
elimu nchini.
Akizungumza na
mwandishi wa gazeti hili hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo
alhaji Suleiman Seif alisema watanzania
wenye moyo wa uzalendo amewaomba kujitokeza katika ujenzi wa chuo.
Taasisi hiyo
iliyosajiriwa miaka 25 iliopita kwa jina la The Registered Trustees of Masjid
Ridhwaa(RTMR) yaani Bodi ya Wadhamini ya Ridhwaa Seminari ikiwa na lengo la
kujenga mskiti,kujenga vituo vya afya,vituo vya elimu na kuendesha miradi ya kiuchumi
kwakuzingatiamisingi ya kiislaam.
Baada ya mafanikio
makubwa Taasisi hiyo iliyo yapata kwakupitia shule ya Ridhwaa,Taasisi hiyoina
wiwa kuanzisha Chuo kikuu ambacho kitatutumika kuelemisha umma kwamapana zaidi
nakuzalisha wataalamu katika nyanja mbali mbali nchini.
Hata hivyo Katibu
wa Bodi hiyo Sheikh Abdul Rashid amesema kuwa ili kuunga mkono kauli ya Rais wa
awamu ya tano Mh John Pombe Magufuli kuelekea uchumi wakati na wa viwanda.
"Pamoja
nakwamba Taasisi yetu toka kuanzishwa kwake ilikuwa na malengo ya kimkakati ya
kuanzisha Chuo kikuu cha aina yake lakini tumeona tuendane na
kasi ya Mh Rais ili
kabla hajaondoka madarakani Chuo hicho kitakacho tambulika kwa jina la Musilim
University of Tanzania (Chuo Kikuu Cha Kiislam Tanzania) kiwe kimekwisha
kamilika.
Hadi sasa Mradi wa
ujenzi wa chuo hicho umefanikiwa kukamilisha ghorofa moja kati ya
ghorofa tano zinazo hitajika Sanjari na hilo tayari zipo ekari 23 katika kijiji
cha Kisemvule wilayani Mkuranga kwa ajiri ya maendeleo ya taasisi hiyo.
Katibu
huyo amewataka wasamalia wema na wenye mapenzi na Taasisi hiyo kuwaunga mkono
katika michango ili kuweza kufanikisha ujenzi wa Chuo
hicho ambacho ujenzi wake unakadiriwa kuchukuwa miaka miwili hadi kukamilika
kwake kulingana na upatikanaji wa fedha.
"Rai yangu kwa
wapenda maendeleo,waislaam,Taasisi mbali mbali za fedha na zile zisizo za fedha,serikalini
na hata kwa watu binafsi wanayo nafasi kubwa yakuchangia maendeleo ya chuo
hicho kwani mwisho wa siku kitawafaa watanzania wote."
Mpango mkakati wa
Chuo hicho nikutoa wahitimu watakao jiajiri wao wenyewe, nakutoa ajira kwa
wengine.Huo ndiyo mpango mkakati wa kuanzishwa kwa chuo hicho kulingana na
mabadirikoya soko la ajira duniani.
Ulimwenguni kote
watu wanatoa elimu itakayo mfanya mtu ajiajiri badala yakusubiri ajira toka
serikalini au kwa mabepari ni wakati wa watanzania kuandaa mazingira ya
kujiajiri.
Kutokana na ukweli
usiopingika Taasisi ya Ridhwaa imeona hii ni fursa itakayo saidia vijana wengi
ambao wataondokana na kuzurura na bahasha katika ofisi za umma na binafsikwa
kutafuta ajira.
Chuo hicho
kitakachoaanza na kitivo cha Habari,kitajikita katika kutoa shahada zitakazo shabihiana
na nasoko la kujiajiri na kuachana na mfumo wa sasa ambao haumuandaai mhitimu
kukabiliana na changamoto za ajira.
Kampasi hiyo
inayojengwa Kinondoni Dar es Salaam itakuwa ya ghorofa tano ambapo pamoja na
kuwa na kumbi za kusomea wanafunzi wa shahada ya kwanza ya habari itakuwa na
sehemu ya kufanyia ibada kwa waumini wakiislam yaani masjidi.
Taasisi hiyo katika
kuelekea uchumi wa viwanda imejipanga kuzalisha wataalamu wenye mwelekeo wa
kidijitali yaani mfumo wa vitendo unao shabihiana na na teknolojia za kisasa
zaidi kuliko mfumo wa kianalogia ,haya yote yatafanikiwa tu pale ambapo watanzania
wataunga mkono kwa michango katika ujenzi wa chuo hicho.
Shahada zitakazo
tolewa na chuo hicho zitabadirika kimuundo na kimfumo ili kuendana na kasi ya
kujiajiri nakuachana nazile ambazo zipo katika mfumo wakuomba ajira.
Miongoni mwa
shahada hizo ni B.A Freelance Photo Journalism, hii itamuaandaa mhitimu kulijua
soko la picha kidunia na ni jinsi ganiwatu hulipwa pesa nyingi kutokana na
taaluma ya picha.
Kwani soko la picha
duniani bado lipo kubwa sana hususani katika mfumo
wa Blogs,Tovuti , Magazeti
Mtandaon kwani sekta ya habari inaelekea huko
siku hizi.




