Mashirika Binafsi Yatakiwa Kushirikiana Na Serikali Kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Afisa Wa Polisi Na Mratibu Wa Kituo Cha One Stop Center Kilichopo Katika Hospitali Ya Amana Bi Christina Onyango akizungumza na baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa kituo hicho mapema leo jijini dar es salaam
Na Sala Mlawas
Wito umetolewa kwa mashirika binafsi kushirikiana na serikali
ili kutokomeza ukatili wa kijinsia ambao umekua ni kikwazo kwa wanawake na
watoto kushindwa kutimiza ndoto zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam afisa
ustawi wa jamii wa shirika la CRC Bi, Violeth Chonya alisema iwapo taasisi hizo
zitashirikiana na serikali kupinga ukatili wa Jinsia anaamini kuwa vitendo
hivyo vya ukatili vitakua vimepungua kwa asilimia kubwa .
Aidha bi Chonya ameongeza kuwa wameona kuna umuhimu wa kuanzisha
vituo zaidi vya kutolea huduma ya mkono kwa mkono yaani one stop center
kutokana na kuwepo na uhitaji mkubwa wa saranga na kawe na katika siku zijazo wanatarajia
kuanzisha pia katika Kata ya makumbusho huduma hiyo jambo lililowasukuma kuweka
mradi huo katika Kata ya.
Wakili Wa Kituo Cha Usuluhishi CRC Bi Suzy Charles
Kwa upande wake Afa Wa Polisi Na Mratibu Wa Kituo Cha One Stop Center Kilichopo Katika Hospitali Ya Amana Bi Christina Onyangois alisema kitu ambacho kimewahamasisha kwenda katika Kata ya kawe ni kutafiti wateja watapokeaje huduma hiyo pia kuangalia muitikio wa wananchi katika kuripoti kesi za ukatili wa Jinsia ka
Pia Afisa mradi wa kutoa msaada kisheria pia ni Wakili Wa Kituo
Cha Usuluhishi CRC Bi Suzy Charles mwitenga alisema lengo kubwa ni kuhamasisha
serikali kuanzisha vituo vingi vya one stop center yaan ( mkono kwa mkono )
kila hospitali kama ilivyo hospitali ya Amana katika maeneo mbalimbali nchini tika
kituo cha one stop center .
Bi onyango na wadau wa CRC wanatarajia kuanzisha kituo hiko. ameongeza
kuwa baada ya kuanzisha mradi huo katika Kata ya kawe wamepata wateja wengi
kwani muitiko huo wa wananchi wameona kunahaja kubwa ya kuanzisha kituo cha one
stop center katika Wilaya ya kinondoni kwa kushirikiana.





