Waziri Wa Nishati Awataka Wafanyakazi Wasisherehekee Krismasi Wala Mwaka Mpya

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani
ametoa siku kumi kwa jengo la Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili
kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.
Waziri huyo pia amewataka
watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa
jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali
washughulikie jengo hilo kuvunjwa.
“Nataka kuanzia leo Desemba 22
ndani ya siku sita jengo hili lote libomoke na kwasababu ni majengo
mawili ndani ya siku kumi majengo yote mawili yawe yamebomoka kama mnaona
vigumu kubomoa jengo lenu waambieni TBL ”amesema
Amesema hadi kufikia mwisho wa
mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala
Krisimasi kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco
wanaaza waanze tusiwakwamishe”amesema.
Amesema wananchi wameshabomoa majengo
yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai Januari mosi ataenda
tena kukagua kuona kama agizo lake limefanyiwa kazi.
“Naimani wananchi hawatapata shida
wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya ,kwa hiyo asiruhusiwe mtumishi
yoyote wa Tanesco kwenda nje ya ofisi yake wakati wa sikukuu zote mbili”amesema
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa
Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia agizo la Waziri na wataenda
kulitekeleza kama lilivyo.



