Shaka Amvaa Maalim Seif Wa Cuf
Wakati wananchi wa Jimbo la
Kinondoni wakijiandaa na kampeni za ubunge wa jimbo hilo, Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),
Maalim Seif Shariff Hamad akijiandaa kushiriki kampeni hizo kwanza
awathibitishie wanachama wake ni lini ataapishwa kuwa Rais wa Zanzibar kama
alivyowaahidi.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM,
Shaka Hamdu Shaka amesema hayo jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya kikao
na watendaji wa sekretarieti za Wilaya za Dar es Saalam.
Shaka amesema Maalim Seif ni
miongoni mwa wanasiasa ambao hawapaswi kusikilizwa na wananchi kutokana na
kufanya siasa ionekane ni sehemu ya uongo kwani haaminiki.
“Maalim Seif kwanza awaambie
wale aliowadanganya lini ataapishwa kuwa Rais wa Zanzibar, amewaongopea sana
wanachama wake na sasa amechusha, kelele za kulilia urais wa Zanzibar kwa njia
ya uongo zimezimika, tunamsubiri kwa hamu aje Kinondoani vijana tumejipanga
kushughulika naye,” amesema.
Source Fullhabari Blog



