BAVICHA: Hila Za Kuifuta Chadema Hazitafanikiwa...Na Hakuna Wa Kuifuta Chadema

Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana la CHADEMA, (Bavicha) Patric Ole Sosopi, amesema kuna lengo la kukifuta
Chama hicho kwani nguvu inayotumika kuumiza upinzani hususani CHADEMA ni kubwa
sana.
Katika mkutano na
wanahabari uliofanyika katika ofisi za chama hicho leo , Sosopi amesema, wapo
watu wanaotumwa kuichafua CHADEMA na kupata sababu ya kukifuta chama hicho.
“Tumewapuuza kwa muda
mrefu, tukiamini vyombo husika vitachukua hatua dhidi yake lakini kwa kuwa
wanamtuma anaendelea kuwa salama. Hila za kuifuta CHADEMA hazitafanikiwa. Kama
tulianza na madiwani 3 leo kina zaidi ya madiwani 70 hakitaweza kufutwa kwa
njia yoyote" Sosopi.
Amesema Chadema
inawahakikishia Watanzania kuwa jitihada za kuifuta CHADEMA hazitafanikiwa na
hakuna mtu atakayeifuta CHADEMA.
Sosopi amesema vijana wa
CHADEMA wapo tayari kulaumiwa baadaye lakini siyo kuacha chama hicho kiweze
kufutwa na kusisitiza kwamba vijana wa chama hicho wako imara na hawaogopi
kufa.



