Breaking News

Kilio Cha Wananchi Wa Mbagala Rangi Tatu Chapatiwa Ufumbuzi.

Katibu Wa Umakuta Bwana Yussuphu Malabe 

Na Sala Mlawas
Umoja wa madereva wa mabasi yaendayo kusini mwa Tanzania (UMAKUTA) kuomba wafadhili wajitokeze kwa ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo mkoani katika kituo kilichopo mbagala rangi tatu kwa lengo la kufikia ngazi ya taifa.

Akizungumza Jijini Dar Es Salaam Na Waandishi Wa Habari Katibu Wa Umakuta Bwana Yussuphu Malabe alisema kuwa kituo hicho awali kilikua kikikumbwa na changamoto kubwa za ubovu wa miundombinu kwani wao kama umakuta wamejipanga kutatua kero hizo na kufikia ngazi ya taifa kwani baadhi ya wageni wengi wanaoingia nchini Tanzania watahitaji kituo hicho kiwe ni kivutio katika ngazi ya taifa.

Aidha bwana malabe ameongeza kuwa mpaka kufikia hivi sasa wanahitaji wao kwa kushirikiana na wadau pamoja na wadhamini watashirikiana bega kwa bega kuboresha kituo hiko kutoka katika ngazi ya vifusi na kufikia ngazi ya lami .
Hata hivyo bwana malabe anatoa wito kwa abiria ambao wanalalamika kupotelewa na mizigo yao wao kama umakuta wameweka ulinzi kwa kutoa elimu kwa wasimamizi wa mabasi hayo yaendayo mkoani.

Kwa upande wake mfanya biashara katika kituo hicho bwana Ismaili pengele amesema kuwa kuwa maendeleo yakituo hicho kwa sasa ni mazuri tofauti na Mara ya kwanza kwani sasaivi watu wa mbagala wanaonekana kupata huduma bora tofauti na mwanzo barabara ilikua ni mbovu sana tofauti na sasa.

Pia bwana pengele anatoa wito kwa uongozi wa umakuta waendelee kufanya vizuri katika kituo hicho kwani wao kama wafanyabiashara watashirikiana na uongozi huo kuhakikisha kuwa wanafikia malengo waliojiwekea .