Mama Kanumba Aangua Kilio Stendi Baada Ya Kuona Bango La KANUMBA THE GREAT

Mama
mzazi wa marehemu Steven Kanumba 'Kanumba the Great' ameshangaza wengi
baada ya kuanza kumwaga machozi katika moja ya stand zinazojaza watu jijini Dar
es salaam baada ya kuona bango lenye picha ya mtoto wake katika maeneo hayo.
Mama huyo
ambae alishindwa kuzuia hasira zake na kulia alisema kuwa mara nyingi amekuwa
akiumia sana na kushindwa kujizuia kutoa machozi kila anapoona picha au kitu
chochote ambacho kinamkumbusha mtoto wake.
"Kila
mara nimekuwa nikiziona picha za kanumba katika mabango , lakini sijui kwanini
hii imenifanya nipatwe na uchungu na niishiwe na nguvu kabisa.-Alisema Mama
Kanumba ambae anasema kuwa alikuwa akielekea maeneo ya segerea kwa ajili ya
kurekodi movie.
Kanumba
alifariki miaka zaidi ya mitano iliyopita baada ya kuuawa na mpenzi wake (Lulu
Michae) waliokuwa na mtafaruku na kusababisha mauaji yake pindi walipokuwa
wakizozana.
Hata
hivyo Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baaada ya kukuta na
hatia ya kuua bila kukusudia.



