Mhe Lema Azungumzia Harakati Za Mange Kimambi Kuhusu Tanzania
Mbunge wa
Arusha Mjini CHADEMA Mhe, Godbless Lema amefunguka na kuweka wazi kuwa kama
chama cha siasa hakiwezi kufundisha watu wake kufanya siasa za kuleta fujo bali
uvunjifu wa amani, uonevu ni vitu ambavyo vinaweza kuwafanya watu wapiganie
haki zao.
Lema
amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya CHADEMA
na kusema kuwa wapo watu wengi ndani ya CHADEMA na nje ya CHADEMA ambao
wamekuwa wakilia na kuumia na mambo yanayoendelea nchini ndiyo maaana hata
mwanaharakati Mange Kimambi kupitia mtandao wake wa kijamii amekuwa na nguvu
kwa kuwa kuna watu ambao wanasikiliza kutokana na mambo yanayofanywa na
serikali.
"Yaani
msingi wa kwanza wa Demokrasia ni amani maanake watu washindane kwa hoja sasa
inatosha maanake nini kumekuwepo na vilio vya CHADEMA na wanachama wake kwa
muda mrefu sana bahati mbaya waandishi wa habari mkafikiri vilio hivi vya
CHADEMA, kanisa likafikiri hivyo na msikiti ukafikiri hivyo lakini leo tunalia
pamoja wakiwepo wafanyabiashara sasa leo kilio chetu si pekee yetu ndiyo maana
kanisa limetoa waraka hivi karibuni Katoliki na Lutherani tunategemea BAKWATA
watafanya hivyo hivyo sasa ipo siku na hiyo siku inakuja"
Lema
aliendelea kusema kuwa "Kuna uchungu unakusanyika kwa watu na hawa watu
wanaandamana moyoni ndiyo maana Mange Kimambi yuko Marekani anatumia Instagram
huku anajibiwa na kiongozi, Mwigulu Nchemba, Mambosasa, sasa kama mtu mmoja
yupo Marekani anaweza kuhamasisha Tanzania na kukawa na presure tunayoiona hii
maanake kwamba watu wamechoka, tunasema imetosha lengo la CHADEMA au lengo
langu mimi au lengo la kiongozi yoyote wa CHADEMA si kuona nchi hii haina amani
lakini lengo la Chama Cha Mapinduzi kwa mwelekeo wao ni kuona watu wanaingia
barabarani kwa nguvu kutafuta haki" alisema Lema.



