MSD Yakidhi Viwango Vya Kimataifa Vya Ubora Na Kutunukiwa Ithibati Ya Kimataifa Ya Juu Ya Ubora
Na Sala Mlawas
Bohari ya dawa ( MSD ) imeendelea kukidhi viwango vya
ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi ,utunzaji ,na usambazaji dawa
,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kupata ithibaki ya kimataifa ya
ubora ya daraja la juu iliyojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa
miaka mitatu 2017 hadi 2020.
Akizungumza na
waandishi Wa habari jijini dar es salaam mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa Bw LAUREAN RUGAMBWA
amesema kuwa kwa kupewa ithibaki hiyo uongozi na watendaji wa MSD wameongezewa
chachu ya utendaji,ubunifu,na kuboresha maswala yote yanayohusiana na mnyororo
wa ugavi kwani Nia yao kubwa ni kuwapatia wananchi huduma bora na zenye viwango
kwa wakati na bei pungufu.
Aidha bwana Rugambwa ameongeza kuwa
serikali ya awamu ya tano imeipa kipaumbele sekta ya afya hivyo basi wao kama
MSD inahakikisha kuwa dawa na vifaa vyote muhimu vinavyohitajika vituo vya
kutolea huduma za afya vinapatikanika na vitosheleze mahitaji .
Hata hivyo vifaa vya kuzalishia akina
mama ni moja ya vifaa muhimu vinavyohitajika mama awe navyo anapokua anakwenda
kujifungua kwani serikali imekua ikisisitiza kila mama anaekwenda zahanati au
kituo cha afya kwa ajili ya kujifungua lazima awe na vifaa hivyo.
Bwana Rugambwa amesema wao kama MSD
wataviuza vifaa hivyo vya kujifungulia kwa bei rahisi ukitofautisha na bei za
mitaani kwani wao mfuko mzima wenye vifaa 12 watauza kwa bei ya shilingi Elfu
21000 ili kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anaweza kumudu garama hizo .
Rugambwa ameelezea baadhi ya vifaa
hivyo vilivyopo ndani ya mfuko huo ni pamba kubwa,Mpira wa kuzuia uchafu, taulo
la kike la uzazi,sindano ya kuzui Damu kupotea ,mipira ya mikono ,kibana kitovu
cha Mtoto ,nyuzi ya kushonea pia anawasisitiza mashirika binafsi yaweze
kujitokeza kununua vifaa hivyo ili waweze kusambaza katika vituo vya afya mbali
mbali kwa lengo la kuwaokoa wananchi wenye uwezo wa chini kwani baadhi ya akina
mama wanapoteza maisha kwa ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kujifungulua.



