ASKOFU KAKOBE ATAKIWA KURIPOTI UHAMIAJI JUMATATU

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel
Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema ameitwa kuhojiwa na Idara ya
Uhamiaji siku ya Jumatatu, Aprili 9, 2018.
Akizungumza leo Jumamosi Aprili 7,
2018 Askofu Kakobe alisema ataitikia wito huo.
“Wamenieleza kuwa wananiita kwa
sababu ya mahojiano hivyo nitakwenda tu hakuna shida. Wameniita Uhamiaji mkoa
wa Dar es Salaam,”alisema Kakobe.



