Mbunge Awashukia Walimu Wanaofelisha Wanafunzi Kwa Rushwa Ya Ngono

Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga
amelitaarifu bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, juu ya vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya walimu wa vyuo vikuu hapa nchini, vya kufelisha
wanafunzi wa kike kwa makusudi.
Akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara
ya Elimu na , Goodluck Mlinga amesema walimu hao ambao wanajifanya ni vidume
vya mbegu, hufelisha wanafunzi wa kike ili wawape rushwa ya ngono, kuweza
kuwawekea maksi za ufaulu.
“Kumekuwa na tatizo la vyo vikuu,
wanafunzi wetu wa kike wanapata shida mno, katika vyuo vyetu vikuu kuna walimu
wanajulikana kabisa kuwa hawa walimu ni madume ya mbegu, wanafelisha wanafunzi
wa kike, wanataka wawape rushwa za mapenzi ndio wawafaulishe”, amesema Goodluck
Mlinga
Pia Mheshimiwa Mlinga amesema yupo
tayari kupeleka majina ya walimu hao ambao wapo vyuo vyote nchini kwa Waziri wa
Elimu, ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
“Mheshimiwa Waziri nitashirikiana na
wewe kama utapenda unipe ushirikiano, nitakuletea majina ya vyuo vikuu vyote
Tanzania, ya walimu ambao madume ya mbegu kazi yao ni kufelisha wanafunzi na
kutaka rushwa za ngono”, amesema Mheshimiwa Mlinga.



