News Alerts: Halima Mdee Naye Kapata Dhamana kwa Bondi ya Milioni 20

Mbunge wa Kawe Halima Mdee leo April
3, 2018 alifikiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa
na akina Freeman Mbowe
Mdee yeye alisomewa mashtaka
mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo,
kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo
cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo,
Mahakama imempa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili
watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20 na kuripoti mara moja kila
wiki.
Mahakama imesema haiwezi
kumnyima mshtakiwa dhamana kwa sababu aliruka dhamana ya polisi maana polisi
ni taasisi nyingine na mahakama ni taasisi nyingine, hivyo ikampatia dhamana
mshtakiwa kwa masharti tajwa hapo juu.



