Foundation For Civil Society Watoa Somo Kuelekea Uchaguzi Nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa
Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi mbele ya
wageni waalikwa ijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano
wa kujadili nafasi ya Asasi za kiraia katika chaguzi zijazo hapa nchini.
Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kujitoa katika
kuhakikisha wananchi wanashiriki kwa wingi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ya
serikali za mitaa na wa serikali kuu wa mwaka 2020.
Hayo yamesemwa mapema leo Jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga
alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi, wenye lengo la kujadili hali
ilivyo kabla ya kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika
hapo mwakani.
Mzee Gallus Abeid kutoka
Mwalimu Nyerere Foundation akichangia mjadala mapema leo jijini Dar es salaam
katika Mkutano wa Uchaguzi ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la
Foundation for Civil Society.
Katika Mkutano uliowakutanisha wadau kutoka Asasi
mbalimbali za Kiraia, Taasisi za elimu ya juu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya
dini mashirika yanayoshughulikia amani nchini kujadili nafasi na
wajibu wao kama azaki kuelekea chaguzi zijazo hapa nchini.
Bwana Kiwanga amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika
kupiga kura umekuwa ni mdogo sana kwani 2010 wamepiga asilimia 43 peke yake na
kwa mwaka 2015 ni asilimia 67 ya wananchi wote wenye sifa za kupiga kura.
Baadhi ya washiriki kutoka
asasi mbalimbali za kiraia wakifuatilia kwa umakini mkutano.
Ameeleza kuwa hii inatokana na wananchi kutokuwa na imani na viongozi wanaochaguliwa kwani wanaamini hata usipopiga kura basi mgombea wa chama fulani atapita kwa njia yeyote ile, hivyo taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya tamisemi na NEC pamoja na ZEC kuboresha utendaji wao wa kazi ili kurejesha imani hiyo kwa wananchi.
Amesema kuwa asasi za kiraia zina jukumu kubwa
la kushirika katika mchakato kabla, kipindi chenyewe cha uchaguzi na baada ya
uchaguzi kwa kuwapa hamasa wananchi lakini pia kuomba nafasi za uangalizi
katika kipindi hicho.
Wageni waalikwa wakifuatilia
mkutano kwa umakini.
Amesistiza uhalali wa kuwapata viongozi ambao ni matwakwa
ya wananchi kwani hii inaweza kuleta kitu kizuri kwa kuwa atakuwa kapewa Baraka
zote na wananchi na pia watashirikiana nae kwa hali na mali kwa kuwa wanajua
ndio chaguo lao sahihi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano
wa uchaguzi ulioandaliwa na shirika la Foundation for Civil Society wakiwa
katika picha ya pamoja jijini Dar es salaam.
Amesema kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo inapotokea watu wanamchagua mgombea Fulani alafu matokeo yanabadilishwa na kupewa mtu mwingine hii sio sawa na inaweza kutowesha amani ya nchi
Lakini pia hali ya mtu anatumia muda mwingi kwenye foleni
ya kujiandikisha na mwisho wa siku anaenda kupiga kura anaambiwa jina lako
halipo kwenye daftari hali hii inasababisha watu wengi kuacha kujiandikisha
kupiga kura na kupoteza haki yao ya msingi.



