Kamanda Mambosasa Azungumzia Mabilioni Ya Dk. Shika

Kamanda wa polisi
kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema suala la Dk. shika
kuingiza pesa zake Tanzania hana uhakika nalo na mtu kutumiwa hela kihalali si
kosa
Amesema kuwa kama
taarifa hizo ni za uongo anaweza kupuuzwa ila endapo kauli yake italeta madhara
basi hatua zitachukuliwa.
Mambosasa
amezungumza hayo leo pindi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari akitoa
ripoti za jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa mbambali kwa kufanya makosa
ya unyang’anyi kwa kutumia silaha za moto.
”Mtu kutumiwa hela
kama ni halali haziingii kwenye pesa ambazo zinatakatishwa au hela ambazo
zinapatikana kwa njia isiyo halali si kosa lakini kama ni muongo tu anajisema
basi kuna mawili anaweza kupuuzwa lakini kama kauli zake zitamwaathiri yeyote
anaweza kuja kulalamika na jeshi la polisi likachukua hatua” amesema Mambosasa.
Mambosasa
amezungumza hayo pindi alipokuwa anajibu swali la mmoja wa waandishi wa habari
baada ya kuhoji juu ya uhalali wa pesa za Dk. Luis Shika ambaye hivi karibuni
taarifa zimeeleza tayari ameingiza mabilioni yake ya fedha nchini Tanzania.
Siku chache
zilizopita Dkt. Louis Shika alivieleza baadhi ya vyombo vya habari nchini juu
ya ujio wa fedha zake na baadhi ya vipande vya dhahabu zilizokuwa nje ya nchi
kuwa tayari zimewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa
ajili ya kuhakikiwa.
Taarifa hizo
zilizua mjadala mkubwa mtandaoni ambapo watu walionesha kutokuamini kwa ujio
huo wa pesa za Dk. Shika wakidhani ni stori zisizo na ukweli ndani yake.
Hata hivyo Shika
alithibitisha ujio wa mali hizo na kuonyesha baadhi ya nyaraka zinazothibitisha
umiliki wa mali hizo



