Kutoka Mwanza: Mwanafunzi Afariki Kwa Kulipukiwa Na Betri Ya Simu.

Mwanafunzi wa
darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto Baraka (13)
amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa akiiunganisha na
radio chakavu.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo ambapo amesema limetokea
Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza.
“Baada ya kutoka
shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa
kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia
mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake," amesema Kamanda
Msangi.



