Breaking News

STAR OIL Yajitosa Kukarabati Barabara Katika Kata Ya Kurasini.

Diwani Wa Kata ya kurasini Mhe. Claudelias Togocho akifafanua jambo kuhusu ukarabati wa barabara hiyo.

Na Sala  Mlawas:
Wito umetolewa kwa Makampuni, Mashirika Na Taasisi nchini kuiga mfano wa kampuni ya STAR OIL iliyopo Kata ya kurasini jijini Dar Es Salaam kwa kujitoa kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao kitendo kitakachosaidia kutatua changamoto mbali mbali hususani miundombinu ya barabara katika Kata hizo.

Diwani Wa Kata ya kurasini Mhe. Claudelias Togocho alisema endapo taasisi na makampuni yatajitokeza kufanya wawekezaji kama ulifanywa na kampuni ya STAR OIL kukjenga miundombinu ya barabara katika kata hiyo kutasaidia kuongeza kasi ya maendeleo nchini ukidhingatiwa kurasini ni Kata mama ambayo ina viwanda vingi vipo katika Kata hiyo.

Alisema kitendo cha kampuni ya STAR OIL kukarabati barabara yenye urefu wa mita mbili na nusu ujenzi ambao gharama kubwa sana hiyo ni chachu ya kuchochea maendeleo katika taifa letu.

"Katika kata hii kuna Makampuni mengi hususani ya wakandarasi lakini hawana mchango mkubwa kama walioonyesha kampuni ya STAR OIL bali wanategemea serikali inabidi tuisaidie serikali sio kila kitu ifanye serikal” Alisema Bw. Togocho.
Related image
Mapema akizungumza Afisa Uajiri Wa Kampuni ya STAR OIL Bi. Estar Doto ameushukuru uongozi wa Kata ya kurasini kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi chote kutatua changamoto ya barabara hiyo wameshirikiana na uongozi hao mpaka kupata kibali ili kukarabati barabara hiyo ufanyike.

Alisema Kampuni ya STAR OIL inatambua jitihada zinazofanya na serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero mbalimbali kuelekea tanazania ya viwanda hivyo wameona wainge mkono kwa kuikarabati kwa kiwango kizuri barabara hivyo ambayo itakua chachu ya kukuza biashara jambo ambalo ni kikwazo kwa wateja kutokana na ubovu uliokisiri katika barabara hiyo.
"Tunaiomba serikali na wadau mbali mbali waliopo katika eneo hili watusaidie kuhakikisha kuwa tunafikia lengo tulilokusudulia ili kuondokana na kero kubwa inayotukabili” Alisema Bi. Doto.

Nao wananchi wa Kata hiyo wameupongeza uongozi kampuni ya STAR OIL kwa kukarabati barabara hiyo kwani ilikuwa kero kubwa hasa kipindi hiki cha mvua hivyo kumwomba waziri wa ujenzi Mhe. Makame Mbarawa kutembelea eneo hilo kujionea hali halisi.