Taarifa Muhimu Toka IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John
Magufuli amemteua Prof Andrew Barnabas Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi
John Kijazi kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa
uteuzi wa Prof. Pembe umeanza siku ya leo.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Pembe alikuwa
Mhadhiri na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia taaluma,
utafiti na ushauri.




