Breaking News

MUSIBA: Na Taarifa Kuwepo Kundi La Vijana Kuandaliwa Kufanya Hujuma kesi Ya Mhe Mbowe.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya CZ na mwanaharakati bw Cyprian Musiba ametoa wito kwa Vyombo vya ulinzi na Usalama nchini kuchukua taadhali katika kipindi chote cha kesi inayoendelea mahakamani ya kiongozi wa kambi ya upinzani nchini mhe. Freeman Mbowe.

Akizungumza mapema leo jiji dar es salaam bwana Musiba alisema kwa Mujibu wa taarifa alizonazo upo mpango umeandaliwa wa kuhujumu na kufanya vurugu mahakamani wakati wa kesi hiyo ikiendelea.

"Ninazo taarifa za kuwepo kwa vijana ambao wamesafirishwa kutoka katika mikoa ya Mara na Tarime zaidi ya 100 kuja jijini dar es salaam kufanya fujo mahakamani wakati shauri hilo likiwa linaendelea" Alisema bw. Musiba.

Alisema vijana hao kwa Mujibu wa taarifa alizonazo tayali wamesha wasili jijini dar tangu juzi Novemba 27 kwa ajili ya kutekeleza hujuma hiyo kipindi ambapo kiongozi huyo akifikishwa mahakamani.

Bw musiba aliongeza kuwa pamoja na kuvishauri vyombo vya ulinzi na Usalama kuchukua taadhali pia ametoa Rai kwa vijana wote nchini kuwa waangalifu na watu, viongozi ambao wamekuwa wakiwa tumia kwa malahi yao binafsi kwa kuanza kufikilia athari ambazo familia yake itazipata ikitokea wakapatwa na matatizo.

"Natoa Rai kwa vijana wote nchini hususani awa ambao wameletwa kutekeleza hujuma hii kujiuliza na kutafakali kwa makini matatizo yoyote watakayokutana nayo waathirika wakubwa ni familia zao." Alisema bw Musiba.

Aidha bw. Musiba pia amewataka wale wote ambao wamekuwa wapo ndani ya chama cha mapinduzi CCM na kuwa na mkakati na kufanya vikao vya siri kutaka kumkwamisha mhe Rais Magufuli kutekeleza wajibu wake taarifa zao anazo na kuwataka kuacha mara moja kwakuwa Rais Magufuli anatekeleza majukumu yake kwa kufata sheria na kanuni kwa Mujibu wa katiba ya nchi.

"Kuna magenge ndani ya chama yanafanya vikao kwa lengo la Kujipanga safu zao za uongozi kuelekea uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na ule wa ubunge na urais hivyo wamekuwa wakifanya hujuma za kukwamisha mhe Rais Magufuli kuteleza wajibu wake wa kutumika watanzania kwa kuwaletea maendeleo taarifa zao Ninazo ivyo ntawapa onyo kuacha mara moja" Alisema.